Wasimamizi wa uchaguzi wa Nov 27 watakiwa kutopuuzia malalamiko yaliyojitokeza
11 December 2024, 5:59 pm
Pamoja na hayo washiriki wa kongamano hilo wamekumbushwa wajibu wao kwa wananchi na kuheshimu katiba na sheria ili kutoa huduma bora kwa watanzania.
Na Yussuph Hassan.
Watendaji na wasimamizi wa uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika Nov 27, 2024 wametakiwa kutopuuzia malalamiko na changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi huo.
Wito huo umetolewa na Jaji Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu za Utawala Bora Matthew Mwaimu katika kongamalo la maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binaadamu liliofanyika Jijini Dodoma.
Mhe mwaimu amesema kwa kufanyia kazi changamoto hizo itasaidia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa TAKUKURU Neema Mwakalyeye amesema kuwa kupitia hotuba ya Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu za utawala bora Matthew Mwaimu amesema watafanyia kazi yote yaliyoelezwa.