Dodoma FM

Ubovu wa barabara za mtaa wakwamisha shughuli za maendeleo Msangalalee

11 December 2024, 4:57 pm

Picha ni eneo la mtaa huo ambalo limechimbika kutokana na mvua zinazo endelea kunyesha ambalo ni eneo la barabara.Picha na Ramadhan Idd.

Mtaa wa Msangalalee wenye wakazi wapatao 20,378, kwa sasa hauna mawasiliano ya baadhi ya barabara kutokana na mvua kuharibu madaraja manne, hali inayosababisha changamoto kubwa kwa wananchi wa eneo hilo.

Wananchi wa Mtaa Msangalalee kata ya Dodoma Makulu, Jijini Dodoma wameomba kurekebishiwa mawasiliano ya barabara za mtaa huo zilizoharibiwa na mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni.
Taswira ya habari imefika katika mtaa huo na kushuhudia baadhi ya miundombinu iliyoharibika hali ambayo inatajwa kukwamisha shughuli za maendeleo.

Sauti za wananchi.

Mwenyekiti wa mtaa huo Leonard Hezron ameiomba serikali kujenga miundombinu imara kwenye barabara za mtaa huo ambazo zimeathiriwa na Mvua.

Sauti ya Leonard Hezron.
Picha ni eneo la daraja likiwa limeharibiwa na mvua katika eneo la Msangalee.Picha na Ramadhan Idd.

Kutokana na athari hizo na zinazoendelea kujitokeza katika miundombinu ya barabara kwa baadhi ya mitaa Jijini Dodoma, Wakala wa Barabara za Vijini na Mijini (TARURA) kupitia mtaendaji wake mkuu Mhandisi Victor Seff hapa anaeleza mikakati iliyowekwa kwa ajili ya kukabiliana athari zinazoendelea kujitokeza.

Sauti ya Mhandisi Victor Seff.