Mvua yakwamisha baadhi ya shughuli Majeleko
10 December 2024, 4:29 pm
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Majeleko wakizungumza na Taswira ya Habari wameelezea hali ilivyo kwa sasa.
Na Victor Chigwada.
Wakazi wa kijiji cha Majeleko wilayani Chamwino wameshindwa kufanya baadhi ya shughuli kutokana na Mvua zinazo endelea kunyesha na kuharibu miundombinu ikiwemo barabara za eneo hilo.
Hayo yanajiri baada ya Mkoa wa Dodoma kushuhudia mvua za masika ambazo katika baadhi ya maeneo zimesababisha uharibifu wa makazi ya watu pamoja na uharibifu wa miundombinu ya barabara.
Wakati huo huo wakazi wa kijiji cha chinangali (i) wao wamesema kuwa athari zilizo sababishwa na mvua zimepelekea wanafunzi kushindwa kufika shuleni na kukosa masomo.
Nae Diwani wa Kata ya Majeleko Musa Omary amekiri uwepo wa changamoto hiyo na kueleza kuwa wameendelea kufikisha taarifa hiyo kwa wakala wa barabara za vijijini na Mjini TARURA.
Amesema wameendelea kuchukua hatua za kukabiliana na wingi wa maji katika baadhi ya barabara .