Wananchi watakiwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya mvua
10 December 2024, 4:04 pm
Hii inajiri baada ya mfululizo wa vipindi vya mvua kunyesha bila kumpuzika hususani katika kipindi hiki cha msimu wa mvua.
Na Nazael Mkude.
Wito umetolewa wakazi wa mtaa wa bwawani kata ya ipagala mkoani Dodoma kuhakikisha kuwa wanachukua tahadhari kwa kipindi hiki mvua zinapoendelea kunyesha.
Wakizungumza na kituo hiki wakazi hao wa mtaa wa bwawani wamesema kwa sasa mvua zimekuwa hazina ratiba maalum za kunyesha hivyo zinaharibu miumbombinu ya bara bara na kusababisha madhara ya maji kuingia katika makazi ya watu.
Akitolewa ufafanuzi huo, mwenyekiti wa mtaa wa bwawani kata ya ipagala bw John komba amesema wananchi wanapaswa kuwa makini na kuchukua tahadhari hasa katika muendelezo wa zinazoendelea kunyesha kwa baadhi ya maeneo hapa nchini.