Dodoma FM

Wakazi wa Bahi road walalamika kero ya maji taka

3 December 2024, 11:56 am

Picha ni chemba iliyo furika maji taka katika eneo la Bahi road .Picha na Mariam.

Hali hiyo inahatarisha usalama wa afya za wananchi katika eneo hilo.

Na Waandishi wetu.

Wananchi wa Mtaa wa Bahi Road Jijini Dodoma  wamepaza sauti zao juu mitaro inayotiririsha majitaka na chemba katika maeneo yao.

Wakizungumza na taswira ya habari wamesema kuwa  hali hiyo inahatarisha usalama wa afya zao hasa katika kipindi hiki cha mvua.