Dodoma FM

Ukali kupitiliza wa wazazi watajwa kuwaathiri Watoto kisaikolojia

3 December 2024, 11:11 am

Picha ni Bi. Veronica Kazungu Kamanda wa polisi kutoka Dawati la Jinsia Dodoma akiongea na Dodoma Tv.Picha na Annuary Shaban.

Wazazi wameombwa kutoa taarifa kwa haraka katika vyombo vya sheria endapo atagundua mtoto amefanyiwa ukatili.

Na Anwary Shaban .                   

Imeelezwa kuwa kutokuwa na uhusiano mzuri  kati ya wazazi na watoto ni chanzo cha Watoto kushindwa kuwa karibu na wazazi wao.

Hali hii pia inatokana na baadhi ya wazazi au walezi kuzungumza na Watoto kwa lugha ya matusi au lugha ya ukali.

Bi. Veronica Kazungu Afisa Dawati la Jinsia Dodoma amesema ukali uliopitiliza kwa wazazi unawafanya Watoto waathirike kisaikolojia na kushindwa kuzungumza na wazazi kuhusu changamoto wanakumbana nazo.

Sauti ya Bi. Veronica Kazungu.
Picha ni Monica Raphael Mkaguzi Msaidizi wa Polisi akiongea na Dodoma Tv.Picha na Annuary Shaban.

Naye Bi. Monica Raphael Mkaguzi Msaidizi wa Polisi amesema kuwa ni vyema wazazi kujenga tabia ya kuwa karibu na Watoto wao ili kutambua changamoto wanazokumbana nazo.

Sauti ya Monica Raphael .