Dodoma FM

Polisi kuadhimisha ya siku 16 za kupinga ukatili Tarime, Rorya

2 December 2024, 10:44 am

Picha ni Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Misime.Picha na Jeshi la Polisi.

Msemaji wa Jeshi hilo pia amesema kuwa Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wananchi wote kutumia maadhimisho hayo kushirikiana kwa dhati ili kutokomeza vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia.

Na Mindi Joseph.
Jeshi la Polisi nchini limesema katika kushiriki maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa mwaka 2024 litashirikiana na wadau mbalimbali kufanya maadhimisho hayo katika Kanda Maalum ya Kipolisi Tarime Rorya ambapo jumla ya watoto 184 waliofanyiwa vitendo vya ukatili wameokolewa na Jeshi hilo

Akitoa taarifa hiyo Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Misime amesema kuwa Jeshi la Polisi limeamua kuadhimisha siku hizo 16 katika mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya ambapo maafisa, wakaguzi na askari wengine wanaofanya kazi katika madawati ya jinsia na watoto Tanzania Bara na Zanzibar sambamba na wakaguzi wa kata za Tarime Rorya, Serengeti na Butiama wataweka kambi.

Sauti ya Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Misime.

Amesisitiza pia tangu maadhimisho haya ya siku 16 yalipoanza Novemba 25.2024 Jeshi la Polisi limefanikiwa kuokoa watoto zaidi ya 184 ambao walikuwa wameandaliwa kukeketwa mwezi wa Desemba 2024 na kwa kushirikiana na wadau wengine wamehifadhiwa sehemu maalum wakati hatua zingine za kisheria zikiendelea