Shule zatakiwa kuajiri mtaalam wa mazingira
2 December 2024, 9:43 am
Hayo yamejiri wakati wa mahafali ya 2 ya shule ya msingi na Awali ya English medium Bahi ambapo Wanafunzi 37 wamehitimu darasa la Awali na kutunukiwa vyeti Wavulana 16 na wasichana 21.
Na Anselima Komba
Mkurugenzi Mtendaji Halimashauri ya Bahi Zaina Mlawa Amezitaka shule zote za Bahi Msingi na Sekondari kuajili mtu wa mazingira kwa lengo la utunzaji wa mazingira ya shule na mwonekano nzuri wa shule kuwa na maji ya uhakika ,kupanda miti na nyasi.
Kwa upande wa Afisa Elimu msingi wilaya ya Bahi Boniface Wilson ameipongeza kamati ya shule Bahi kwa kuendelea kupigania nizamu na maendeleo ya Elimu na kuhakikisha Bahi inaendelea kufanya vizuri kielimu kuanzia ngazi ya wilaya,mkoa .
Pamoja na hayo Shule ya English medium Bahi inakabiliwa na changamoto za uhaba wa madarasa na nyumba za walimu Nyemo Bendera mwanafunzi wa Darasa la pili amesema hayo alipokuwa akisoma risala kwa Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mtendaji Bahi Zaina Mlawa.
Nao Wazazi walezi katika shule hiyo Liberatha Sunday na Kudra Kitabuge wameomba ushirikiano wa mzuri baina ya wazazi na Walimu kwa ulinzi na usalama malezi bora ya watoto kuanzia ngazi ya familia hadi shule.