Dodoma FM

Dodoma yaendelea kuwavutia wawekezaji

1 December 2024, 2:14 pm

Picha ni baadhi ya wageni walio hudhuria katika ufunguzi wa Wheel Algiment Jijini Dodoma. Picha na Fred Cheti.

Jiji la Dodoma linaendelea kuwataka wawekezaji wengine kuja kuweza Dodoma.

Na Mariam Kasawa.
Jiji la Dodoma limetajwa kuwa mahali sahihi pa uwekezaji hivyo wawekezaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wametakiwa kuja kuwekeza katika mkoa huu.

Serikali imeendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji ili kuwavutia wawekezaji kuwekeza hapa nchini hususani katika jiji la Dodoma kwani kuna fursa nyingi ambazo zimeletwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan.

Miongoni mwa wawekezaji walio vutiwa kuja kuwekeza Dodoma ni kampuni ya Wheel Aligment ambayo ni kampuni inayo husika na ufundi wa magari.

Picha ni Afisa ya habari wa Kampuni ya Wheel Aligment Bw. Criss Mendoza akiongea na Dodoma Tv. Picha na Fred Cheti.

Akiongea na Dodoma Tv Afisa ya habari wa Kampuni ya Wheel Aligment Bw. Criss Mendoza anasema wamevutiwa kuwekeza katika Jiji la Dodoma kutokana na fursa zinazo patikana katika mkoa huu huku akieleza ujio wao na vifaa vya kisasa katika utengenezaji wa magari.

Sauti ya Bw. Criss Mendoza.

Nao baadhi ya mafundi wa kampuni hiyo wakaeleza jinsi walivyo jiandaa kuwahudumia wananchi.

Sauti za mafundi.