Paranga Chemba walilia zahanati
14 November 2024, 8:06 pm
Na Yussuph Hassan,
Wakazi wa kijiji cha Paranga Wilayani Chemba Mkoani Dodoma wapo tayari kuchangia nguvu zao ili kufanikisha ujenzi wa zahanati ili kuondokana na changamoto ya wanawake kujifungulia njiani.
Hatua hii inajiri baada ya kufikiwa na mradi wa ninawajibika unaotekelezwa na taasisi ya Wajibu kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la AFNET ,lengo likiwa ni ushiriki wa wananchi katika miradi ya maendeleo
Baadhi ya wanawake akiwemo Aisha Salum,Maria Tula na Halima Abdalah wamesema kutokana na ukosefu wa zahanati kijijini inalazimu kutumia dawa za miti shamba ili kupata ahueni ya matibabu.
Fatma Juma ni moja ya mwanamke ambaye alijifungualia njiani kutokana na ukosefu wa zahanati katika kijiji hicho anazeleza juu ya kisa hicho.
Kwa upande wake Agida Omary Ford ambaye ni afisa Mipango kutoka halmashauri ya Wilaya ya Chemba anaelezea hatua ambazo watachukua baada ya wananchi hao kuibua changamoto ya ukosefua kituo cha afya.
Awali Mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la AFNET Joy Njelango ameelezea umuhimu wa jamii kushiriki katika kuibua changamoto zinazowakabili ili ziweze kuweka kwa mpango wa kata kwa ajili ya utekelezaji.
Tangu kijiji hicho kuanzishwa mwaka 1970 hakijawahi kuwa na zahanati hali inayokwenda tofauti na Sera ya Afya ya Juni 2007,ambayo inaeleza kuwa zahanati inapaswa kuwapo kwenye kila kijiji na kituo cha afya kwa kila kata.