Dodoma FM
Uelewa matumizi ya mfumo yanyima makundi maalumu 30%
14 November 2024, 8:06 pm
Na Mariam Kasawa.
Jamii ya kundi maalumu imetajwa kukabiliwa na changamoto ya uelewa jinsi ya kutumia mfumo wa Serikali wa NEST ili kupata taarifa za kiuchumi
Bi .Felister Mdemu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wanawake na Makundi Maalum anasema asilimia 30 iliyotengwa na serikali kwaajili ya wanawake haitumiki kutokana na uelewa mdogo wa kuingia kwenye mfumo wa huo.
Kutokana na changamoto hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Bi. Mwajuma Hamza anasema wamejipanga kuwafikia wafanyabiashara na wajasiliamali pamoja na makundi maalumu kuwatia elimu jinsi ya matumizi ya mfumo huo.
Baadhi ya vijana na wanawake wanaeleza changamoto zinazo wakabili ikiwa ni pamoja na uelewa mdogo.