Dodoma FM
Upimaji afya ni muhimu kubaini viashiria vya magonjwa yasiyoambukiza
14 November 2024, 8:06 pm
Na Anselima Komba
Maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukiza yameanza rasmi Novemba 9/11/2024 na yatahitimishwa Novemba 16/11/2024 huku yakibeba kauli mbiu isemayo muda ni sasa zuia magonjwa yasiyoambukiza mahali pa kazi
Dkt Rhoda Rameck ambaye pia ni Mratibu wa magonjwa yasiyoambukiza katika Wilaya ya Bahi amewataka wananchi kujiwekea utamaduni wa kwenda hospital kupima afya zao mara kwa mara ili kuepuka athari za magonjwa hayo.
Kwa upande wa wananchi ambao wamejitokeza katika viwanja vya Singidani katika maadhimisho hayo ili kupata huduma ya upimaji wa viashiria vya magonjwa yasiyoambukiza wampongeza jinsi ya utaratibu mzuri wa utoaji wa huduma.