Matumizi ya nishati safi yashika kasi sehemu za umma
13 November 2024, 5:24 pm
Na Mariam Kasawa.
Hivi karibuni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizitaka taasisi zinazo pika chakukula kwa watu zaidi ya 100 kuacha matumizi ya kuni na mkaa na kuhamia kwenye nishati safi hadi hadi kufikia Disemba 30, 2024.
Akiwa jijini Dodoma, Waziri Mkuu alibainisha taasizi zinazotakiwa kuachana na matumizi ya mkaa na kuni na badala yale waanze kutumia nishati safi ikwemo gesi.
Katika kuitikia wito huo, zaidi ya Sh 40 milioni kuweka miundombinu ya majiko yanayotumia nishati safi ya gesi katika Shule ya Sekondari Morogoro na Kituo cha Kulelea Wazee cha Fungafunga.
Maria Samweli ambaye ni mpishi katika Shule ya Sekondari Morogoro amebaibisha gharama waliyokuwa wanatumia kwa manunuzi ya nishati na hata baada ya kuanza kutumia nishati mbadala.
Akizungumza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dk James Mataragio, kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Dotto Biteko, amezitaka mamlaka za nishati, kama Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kushirikiana na jamii kutoa elimu juu ya faida za nishati safi.