Dodoma FM

Soko la Machinga Dodoma kufanyiwa maboresho

29 October 2024, 8:04 pm

Na Anwary Shabani.                                                                         
Soko la Machinga Jijini Dodoma litafanyiwa maboresho ya uwekaji wa vigae vya chini ili kuondoa vumbi ambalo limekuwa kero kwa wafanyabiashara sokoni hapo.

Maboresho hayo yanafuatia baada ya malalamiko toka kwa wafanyabiashara wadogo wadogo katika risala iliyosomwa  na Katibu wa soko la  Machinga Bwn. Mark Mwagale mbele Mbunge wa jimbo la Dodoma na Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde na Mkuu wa Wilaya Mhe. Jabir S hekimweri.

Pichani Katibu wa soko la  Machinga Bwn. Mark Mwagale akisoma risala mbele Mbunge wa Jimbo la Dodoma na Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde katika mkutano wa hadhara soko la Machinga.
Sauti ya Bwn. Mark Mwagale

 Akijibu risala hiyo Mbunge wa Jimbo la Dodoma na Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde anaeleza jinsi serikali itakavyoshughulikia changamoto hiyo.

 Pichani Mbunge wa Jimbo la Dodoma na Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde akijibu risala ya wafanyabiashara katika soko la Machinga.
Sauti ya Mhe. Antony Mavunde

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mh Jabir Shekimweri amewaeleza wafanyabiashara hao jinsi wanavyoweza kubadili changamoto kuwa fursa.

Pichani Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mh Jabir Shekimweri akiongea na wafanyabishara katika soko la Machinga.
Sauti ya Mh Jabir Shekimweri

Mkutano huo uliowakutanisha wafanyabiashara mbalimbali wa soko hilo umeambatana na zoezi la kugawa majiko kwa mama lishe ikiwa ni kuunga mkono juhudi za matumizi ya nishati safi nchini Oktoba 29. 2024.

Pichani baadhi ya mamalishe waliohudhuria mkutano wa wafanyabiishara soko la Machinga