DUWASA yaondoa adha ya maji Kisasa
29 October 2024, 4:00 pm
Na Selemani Kodima.
Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Dodoma DUWASA imekamilisha uchimbaji wa kisima cha maji kitakachowahudumia wananchi wapatao Elfu 28 jijini Dodoma katika maeneo ya Kisasa, Mwagaza na Nyumba Mia Tatu na utatekelezwa kwa kipindi cha wiki nne.
Uchimbaji wa kisima hicho uliotekelezwa kawa wiki nne, umakamilisha idadi ya visima 10 vilivyochimbwa pembezoni ya mji ili kuondoa adha ya maji kama anavyoeleza Mwakilishi wa Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira , Meneja Miradi DUWASA Mhandisi Norbet Mwombeki .
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Alhaji Jabir Shekimweri amepongeza utekelezaji wa uchimbaji wa kisima hicho kwa kutumia mapato ya ndani Oktoba 27, 2024 alipotembelea mradi wa maji akiambatana na Mbunge wa jimbo la Dodoma Mhe. Antony Mavunde pamoja na baadhi ya viongozi wa CCM.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini na Waziri wa Madini Mhe Antony Mavunde ameeleza juu ya mataraji ya utekelezaji wa mradi huo.