‘Kuzaliwa kichwa kikubwa siyo laana’
25 October 2024, 6:35 pm
Na Mindi Joseph.
Jamii imetakiwa kuondokana na dhana potofu kuwa watoto wanaozaliwa wakiwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi ni laana au mkosi.
Daktari wa upasuaji wa magonjwa ya ubongo na mishipa ya fahamu kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili Hamis Shaban visababishi vya tatizo la mgongo wazi na kichwa kikubwa.
.
Norbert Kyando kutoka Chama cha Wazazi Wenye Watoto Wenye Ulemavu wa Vichwa Vikubwa na Mgongo Wazi nchini amesema bado kuna mitazamo hasi toka kwa jamii ukiwa na mtoto mwenye ulemavu wa aina hiyo.
Aidha wajawazito wanashauriwa kutumia kwa wingi vyakula vyenye madini ya Folic ili kuepuka kujifungua watoto wenye tatizo la vichwa kikubwa na mgongo wazi.
Kila ifikakpo Oktoba 25 kila mwaka ni maadhimisho ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu wa Vichwa Vikubwa na Mgongo Wazi Duniani. Takwimu za Wizara ya Afya zinaonyesha kuwa kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa nchini, watatu huwa na tatizo la vichwa vikubwa au mgongo wazi ama vyote kwa pamoja.