Zifahamu athari za betri chakavu za magari
23 October 2024, 6:58 pm
Na Mariam Kasawa.
Betri chakavu za magari zimetajwa kuwa na athari kubwa kwa viumbe na mazingira endapo hazitateketezwa katika utaratibu mzuri.
Akizingumza katika wiki ya kujiondosha na kuepukana na kemikali zinazotokana na betri chakavu Bi. Dora Swai katibu mtendaji kutoka Ajenda anasema athari zinazotokana na betri chakavu za magari endapo urejezaji wake utafanyika katika utaratibu usiosahihi.
Aidha Bwn. Jamal Baruti meneja wa tathmini ya athari kwa mazingira kotoka baraza la usimamizi na uhifadhi wa mazingira NEMC ametoa rai kwa wawekezaji pamoja na wamiliki wa viwanda kuzingatia sheria ya mazingira.
Warsha iliyofanyika katika wiki ya kujiondosha na kuepukana na kemikali zinazotokana na betri chakavu iliwakutanisha wadau wa mazingira , wamiliki wa viwanda pamoja na baraza la usimamizi na uhifadhi wa mazingira NEMC mapema wiki hii