Wizara ya Afya yapunguza 70% rufaa za matibabu nje ya nchi
21 October 2024, 7:35 pm
Na Mariam Kasawa
Mpango wa serikali wa miaka mitano 2020-2025 kusomesha wataalam bingwa na wabobezi 300 kila mwaka, umepunguza kwa 70% rufaa za matibabu nje ya nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Waziri wa Afya Mh. Jenista Mhagama anabainisha mipango ambayo wizara imejiwekea ili kuimarisha afya sekta ya afya.
Aidha Mh. Mhagama amesema jitahada hizi zinazo fanywa katika sekta ya afya zinalenga kupunguza rufaa za matibabu nje ya nchi na kupunguza gharama za matibabu.
Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasilimali Watu, Wizara ya Afya Dkt. Saitori Laizer, akajibu baadhi ya maswali yaliyo ulizwa na waandishi wa habari kuhusu rufaa za nje.
Serikali imejiwekea lengo la miaka mitano 2020-2025 la kusomesha wataalamu bingwa na wabobezi wasio pungua 300 kwa kila mwaka wa fedha kupitia ufadhili wa masomo wa serikali unaojulikana kama Samia Health Specialization Scholarship Program.