Dodoma FM

Mfumo dume bado ni changamoto kwa mwanamke kijijini

15 October 2024, 7:29 pm

Na Léonard Mwacha

Ukosefu wa usawa wa kijinsia unaosababishwa na mila na desturi unadhoofisha uwezo kamili wa wanawake wa vijijini kujikwamua kiuchumi.

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya mwanamke anayeishi kijijini na kutambua mchango wake katika uzalishaji wa chakula kwa jamii zao, kulinda mazingira kupitia ustahimilivu wa hali ya hewa, na kukuza uchumi wa maeneo yao bado  kuna ukosefu wa usawa wa kijinsia.

Mwanasheria kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu Euphrasia Pelagio anaelezea jinsi ya upatikanaji wa msaada wa kisheria kwa mwanamke anayeishi kijijini katika mahojiani na Leonard

Leonard Mwacha akiwa katika mahojiano na Mwanasheria kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu Bi, Euphrasia Pelagio .
Sauti ya Leonald Mwacha na Euphrasia Pelagio

Siku ya Kimataifa ya wanawake wa vijijini inalenga kutoa mwanga juu ya nafasi muhimu waliyonayo  wanawake hawa na kupaza sauti ili kuboresha jinsi wanavyotendewa katika kila pembe ya dunia.