Dodoma FM
Ulishaji mifugo holela ni adui wa mazingira
14 October 2024, 7:57 pm
Na Mariam Kasawa.
Wakazi jijini Dodoma wametakiwa kuachana na ufugaji holela ambao umekuwa ukichangia kwa kiasi kikubwa kuangamiza miti inayo pandwa.
Bwn. Innocent Makomba Afisa mazingira amesema hayo katika mahojiano maalum baada ya zoezi la upandaji miti katika shule ya msingi K ndege Oct 10.
Mwenyeki wa mtaa wa K ndege Bw. Innocent Lufyagila amesema kuwa jitihada walizofanya katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira ni pamoja kufanya vikao na wananchi ili kuzungumzia suala la utunzaji wa mazingira.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya K ndege Bw. Albert Mbalanga amesisitiza umuhimu wa upandaji miti kwa jamii.