Fahamu madhara ya vidonge vya P2
9 October 2024, 6:25 pm
Na Lilian Leopord.
Matumizi ya vidonge vya P2 mara kwa mara kama mpango wa dharula wa kuzuia mimba imelelezwa kuwa na madhara makubwa katika suala zima la lafya ya uzazi.
Akiongea na Dodoma TV, Daktari Fransis Mbwilu kutoka katika kituo cha UMATI Dodoma amesema kuwa madhara yanayojitokeza endapo mwanamke atajenga mazoea ya kutumia vidonge vya P2 mara kwa mara ili kuzuia mimba ni pamoja na kupata hedhi isiyo na mpangilio.
Aidha Dkt. Fransis Mbwilu ameeleza jitihada wanazozichukua ili kutoa elimu kwa jamii juu ya matumizi sahihi ya vidonge vya P2 ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza endapo mwanamke atajenga mazoea ya matumizi ya vidonge hivyo.
Wakitoa maoni yao kwa nyakati tofauti, wananchi wameomba elimu zaidi itolewe ili kujua matumizi sahihi ya vidoge vya P2 ili kuepuka madha yanayoweza kujitokeza.