Zijue sheria za mazingira kuepuka adhabu
8 October 2024, 6:40 pm
Na Mariam Kasawa.
Wananchi wametakiwa kuzitambua sheria mbalimbali za usimamizi wa mazingira pamoja adhabu zake endapo sheria hizo zitakiukwa ili kuepuka kuvunja sheria .
Bwn. Onesmo Nzinga mwanasheria kutoka baraza la uhifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC amesma hayo wakati akiongea katika mafunzo ya waandishi wa habari mapema wiki hii.
Aidha meneja wa tathimini ya athari kwa mazingira Bwn. Jamal Baruti kutoka baraza hilo amesisitiza kuwa ni muhimu kwa elimu ya tathmini ya athari kwa mazingira itolewe kwa jamii ili kuwepo na uelewa wa kutosha juu ya sheria za usimamizi wa mazingira.
Kulingana na kanuni ya kupiga marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki na udhibiti wa taka ngumu wananchi wametakiwa kuzitambua adhabu ambazo mtu anaweza kupewa iwapo atakiuka sheria hizo.