Dodoma FM

Kuvunjika kwa ndoa ni pigo kwa watoto

26 September 2024, 7:51 pm

Na Lilian Leopold                

Kutengana kwa wazazi  katika ndoa kumeathiri watoto kwa kiasi kikubwa hasa katika suala la malezi.

Baadhi na wazazi mkoani Dodoma wametoa maoni yao juu ya athari zinazowakabili watoto juu ya kuvunjika kwa ndoa. Wakitaja baadhi ya athari hizo ni pamoja na watoto  kijiingiza katika makundi yasiyofaa, kukosa furaha na wengine kushindwa kupata mahitaji yao ya msingi.

Sauti za wananchi

Aidha  jamii inashauriwa kwa wazazi waliotengana kutokana na changamoto mbalimbali kuhakikisha wanakaa na kumaliza tofauti zao ili  kutasaidia watoto kulelewa katika misingi ya wazazi wote wawili na kunusuru vizazi vya sasa na vizazi vijavyo katika suala zima la maadili

Sauti za wananchi

Malezi bora ya mtoto husaidia kumkuza mtoto katika furaha, amani, usalama, utulivu wa moyo na akili. Jamii inapaswa kuelewa kuwa umuhimu wa malezi bora kumwezesha mtoto kufikia ndoto  zake za maisha.