Dodoma FM

Elimu kipindi cha ujauzito husaidia afya ya uzazi  

23 September 2024, 8:43 pm

Watalamu wa Afya wanashauri muda muafaka wa kuanza kliniki ya afya ya uzazi kwa mama mjamzito ni pale tu anapogundua kuwa ni mjamzito.

Na Yusuph Hassan.

Jamii inashauriwa kuhakikisha kuwa inapata elimu ya afya ya uzazi kabla ya kubeba ujauzito au wakati wa ujauzito ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza kwa mama mjamzito na mtoto aliye tumboni.

Baadhi ya wajazi wa Dodoma wanaeleza umuhimu wa kuwahi mapema kliniki mara baada ya kutambulika kwa uhauzito na msaada ambao mama mhamzito anatakiwa kuupata toka kwa watu wa karibu na jamii kiujumla.

Daktari Joseph Nkusa kutoka Sipha Polyclinic anasema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuchukuwa thadhari dhidi ya viasharia hatari katika kipindi cha ujauzito.

Daktari Joseph Nkusa kutoka Sipha Polyclinic
Sauti ya Daktari Joseph Nkusa
Elimu ya uzazi husaidia mama kujifungua mtoto mwenye afya njema