Dodoma FM

Vijana jiepusheni na rushwa chaguzi zijazo

20 September 2024, 7:50 pm

Na Fred Cheti,

Kuelekea katika chaguzi zijazo vijana wametakiwa kuwa makini na kujiepusha na masuala ya  rushwa katika chaguzi hizo ili kuwapata viongozi wataokaopatikana kwa haki na kuwaletea maendeleo.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imekuwa ikitoa elimu kwa makundi mbalimbali pamoja na kuanzisha kampeni mbalimbali ili kuzuia vitendo vya rushwa kuelekea chaguzi zijazo.

Afisa Rushwa Takukuru Dodoma Bwn. Victor Swela
Sauti ya Bwn. Victor Swela
Henry Mpolo Mkazi wa Dodoma

Baadhi ya vijana jijini Dodoma wametoa maoni yao jinsi wanavyoweza kujiepusha na rushwa katika chaguzi zijazo. Vijana ni kundi ambalo linadaiwa kutumiwa na viongozi au wagombea katika nyaja tofauti kwenye chaguzi.

Sauti ya Ndg, Henry Mpolo na Ndg. Jacksonea Chuma
Jacksonea Chuma Mkazi wa Dodoma

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajia kufanya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu ambapo tayari  imetangaza rasmi tarehe 27 Novemba 2024 kuwa tarehe ya uchaguzi huo pamoja na uchaguzi mkuu mwakani.