Dodoma FM

Namba hairidhishi wanawake nafasi za uongozi

19 September 2024, 7:51 pm

Hali ya mfumo dume , itikadi za kidini na imani ndogo ya jamii kwa mwanamke imepelekea idadi ya wanawake katika nyadhifa mbalimbali kuwa ndogo tofauti na wanaume hapa nchini.

Na Mariam Kasawa

Kupitia utafiti uliofanywa na mtandao wa jinsia tanzania TGNP unaonyesha namba ya wanawake katika uongozi mbalimbali ni ndogo tofauti na wanaume mfano katika uongozi wa ngazi ya vijiji viongozi wanawake ni 246 sawa na asilimia 2.1% huku wanaume wakiwa 11,669 sawa na asilimia 97.9%.

Akiongea katika warsha iliyo wakutanisha wanawake, viongozi wa dini ,viongozi wa vyama vya siasa na mashirika mkuu wa kitengo cha sheria ofisi ya msajili wa vyama vya siasa Bw. Muhidini Mapeyo anasema tamaduni pamoja na woga ni hali inayo pelekea namba ya wanawake kuwa ndogo katika uongozi.

Mkuu wa kitengo cha sheria ofisi ya msajili wa vyama vya siasa Bw. Muhidini Mapeyo anasema
Sauti ya Bw. Muhidini Mapeyo
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Manyara Mh Regina Qwaray

Nao baadhi ya wabunge wanawake walioshiriki katika warsha hiyo mbunge wa viti maalum Mkoa wa Manyara Mh Regina Qwaray na mbunge wa viti maalum mkoa wa Rukwa wanasema mfumo uimarishwe kuanzia kwa wajumbe .

Sauti ya nMh Regina Qwaray

Aidha wanaume walioshiriki walio warsha hiyo kutoka jijini Dodoma wanasema wanawake wanapaswa kujiamini kwamba wanaweza ili kupambana na rushwa katika uchaguzi.

Sauti za washiriki wa warsha