Maelezo na taarifa ya ugonjwa ni wajibu na haki ya mgonjwa
19 September 2024, 7:51 pm
Uelewa wa baadhi ya watu kufahamu haki zao za msingi wanapokuwa katika vituo vya afya na hospitali bado ni mdogo. Hali hii ni kutokana na uhaba wa elimu juu ya suala hilo pamoja na baadhi yao kutokuwa na utamaduni wa kuuliza juu ya huduma wanayopatiwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa Prof. Abel Makubi amewaomba wagonjwa kutoa maelezo sahihi ya ugonjwa na pia na kuwataka kuomba taarifa toka kwa madaktari mara wanapohudumiwa.
Mmgonjwa hapaswi kukubali matibabu bila ya kufahamu kikamilifu maelezo ya kina kuhusu athari zinazoweza kutokea, faida za matibabu na mbadala wa matibabu yanayopendekezwa na pia kuwepo na siri baina ya mgonjwa na daktari
Jamii inashauriwa kutopuuza maumivu au dalili mbaya watakazohisi katika miili yao kwani kunasababisha kuchelewa kupata matibabu ili hali ugonjwa ukizidi kukua na kusababisha athari kwa mgonjwa.
Kila septemba 17 ya kila mwaka ni maadhimisho ya siku ya usalama wa mgonjwa duniani, lengo ikiwa ni kuzingatia usalama wa mgonjwa kwa kuanzisha na kuimarisha mifumo inayotegemea sayansi, kuboresha usalama wa wagonjwa na ubora wa huduma za afya.