“Mwache aongoze”
18 September 2024, 7:42 pm
Na Mariam Kasawa
Baadhi ya jamii zinaamini kuwa mwanamke hana uwezo wa kuongoza hali inayopelekea idadi ya wanawake kuwa chache katika nafasi mbalimbali za uongozi ikilinganishwa na wanaume.
Mashirika yasiyokuwa yakiserikali yameanzisha mradi wa pamoja ambao unalenga kuwaimarisha wanawake na kuwainua kiuchumi, kuelimisha na kuwaibua wanawake ili kuiaminisha jamii kuwa mwanamke anaweza kuongoza sawa na mwanaume .
Mradi huu umekuja na kaulimbiu inayo sema MUACHE AONGOZE ikiwa na mana kwamba mwanamke anaweza hivyo anapaswa kupewa nafasi mbalimbali za kuongoza.
Bi Joyce Peter ni Mwanasheria kutoka Morogoro Paraligo Centre anasema waliona kwenye jamii bado kuna changamoto hivyo kupitia mikakati watakayo iunda itasaidia kuwaibua wanawake ambao watasimama na kugombea nafasi mbalimbali.
Halima Kakolanya mtaalamu wa masuala ya jinsia na ujumuishi kutoka Aghakhan Foundation anasema mradi huu unalengo la kuondoa mila kandamizi ili kumpa nafasi mwanamke kushiriki dhughuli za maendeleo ikiwemo uongozi.
Baadhi ya washiriki wakiwemo viongozi wa siasa waliohudhuria mkutano wa mraadi huo walikuwa na maoni kadha wa kadha.