Je, jamii ina uelewa gani kuhusu saratani ya matiti?
18 September 2024, 7:42 pm
Kwa mujibu wa takwimu za ufuatiliaji wa saratani kupitia ripoti ya utafiti ya Globocan zinaonesha kuwa nchini Tanzania takribani wagonjwa wapya wa saratani elfu 40 hugunduliwa kila mwaka na karibu jumla ya watu elfu 27 wenye saratani hufariki dunia kila mwaka .
Na Yusuph Hassan.
Licha ya elimu kuendelea kutolewa juu ya ugonjwa saratani ya matiti bado jamii imekuwa haina uelewa wa kutosha juu ya ugonjwa huo.
Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Hospitali ya Mkoa wa Dodoma Dkt. Pelauis Kato amaeleza zaidi kuhusu saratani ya matiti ikiwa ni mohja ya jitihada za watabibu katika kutoa elimu.
Nchini Tanzania. inakadiriwa kuwa takribani ya wanawake 25% wamebainika kuwa na Saratani ya mlango wa kizazi ikifuatiwa na Saratani ya matiti kwa 10%.