Dodoma FM

Dunia yaadhimisha siku ya kimataifa ya kuhifadhi tabaka la Ozoni

17 September 2024, 8:59 pm

Serikali imetakiwa kuanzia ngazi ya chini katika maadhimisho mbalimbali yanayo husiana na utunzaji wa mazingira ili kuwajengea uelewa wananchi.

Na Mariam Kasawa

Tanzania imeungana na Dunia kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kuhifadhi Tabaka la Ozoni (Ozone) amapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema kulinda tabaka la ozoni, utawala na utekelezaji ndio nguzo septemba. Maadhimisho hayo yamefanyika 16 Septemba 2024.

Bw. Daruesh Said , mdau wa mazingira ambae ni Mkurugenzi wa Chapakazi group taasisi inayo jihusisha na utunzaji wa Mazingira hapa Jijini Dodoma anasema wanatamani kuona maadhimisho haya ya mazingira yakianzia katika ngazi ya chini kwa wananchi wa kawaida na viongozi wao ili kuwajengea uelewa zaidi.

Mkurugenzi wa Chapakazi group Bw. Daruesh Said
Sauti ya Bw. Daruesh Said

Vijana wanao jihusisha na utunzaji wa mazingira wanasema maadhimisho ya mazingira yaende sambamba na utoaji wa elimu kwa wananchi ili kuwajengea uelewa zaidi .

Mdau wa mazingita toka Chapakazi Group
Sauti ya mdau wa mazingita toka Chapakazi Group

Wananchi wanatamani kupata elimu zaidi ya utunzaji wa mazingira hususani katika ajenda mbalimbali za serikali ikiwemo ajenda ya nishati safi pamoja na uvunaji wa hewa ya cabon ili waweze kunufaika.

Sauti ya mdau wa mazingita toka Chapakazi Group
Picha kuonesha utunzaji wa mazingira