Gharama za umeme ni kikwazo cha maendeleo kiuchumi Ng’ong’ona
17 September 2024, 9:00 pm
Licha ya jitihahada za Wakala umeme Vijijini (REA) kusambaza huduma ya umeme katika vijiji takribani 12,318 , wananchi wa Mtaa wa Ng’ong’ona Jijini Dodoma wamedai kuwa gharama ya kuvuta umeme kwa sasa ni kubwa
Na Mindi Joseph.
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeendelea kuwezesha upatikanaji wa nishati bora maeneo ya vijijini ili kuimarisha maisha ya wananchi kwa kuibua fursa ya shughuli za kiuchumi kama anavyoeoeleza Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy anafafanua Zaidi.
Licha ya jitihahada hizo, Wananchi wa Mtaa wa Ng’ong’ona Jijini Dodoma wamedai kuwa gharama ya kuvuta umeme kwa sasa ni kubwa hivyo imechangia wengi wao kujikuta wakikosa huduma hiyo kusababisha kuwa duni kiuchumi kwa kushindwa kufanya shughuli za kiuchumi.
Wakala wa Nishati Vijijini imekamilisha kufikisha umeme vijiji vyote na sasa imeanza upelekaji umeme katika vitongoji 3,060 nchini.