Dodoma FM

Ijue historia ya kilimo cha mpunga Bahi

10 September 2024, 7:21 pm

Na Yusuph Hassan. Bahi ni moja ya wilaya inayopatikana ndani ya mkoa wa Dodoma umbali wa kilomita  51 toka Dodoma Mjini. Wilaya hii ilijihusisha na kilimo cha mazao mchanganyiko kabla ya kuanza ulimaji wa zao la mpunga  mwaka 1983 kama anavyosimulia mzee Ramadhani Issa mwenyeji na mkazi wa Bahi.

Mzee Ramadhani Issa mwenyeji na mkazi wa Bahi
Sauti ya Mzee Ramadhani Issa mwenyeji na mkazi wa Bahi

Mzee Ramadhani Issa amesema kuwa kilimo cha mpunga wilayani hapo kilianza toka mwaka 1983 baada ya Shirika la Chakula Duniani FAO  kuanzisha mfano wa majaruba takribani 48 na kuyagawa kwa wanachi.

Sauti ya Mzee Ramadhani Issa mwenyeji na mkazi wa Bahi

Katika kutia nguvu kilimo cha mpunga Bahi mwaka 1992,  shirilka la IFAD (The International Fund for Agricultural Development ) lilijitokeza na kuendeleza kilio cha mpunga kwa kutumia nguvu kazi za wananchi. Imeelezwa kuwa toka wakati huo kilimo cha mpunga Bahi limekua ni zao tegemezi kiuchumi kwa wakazi wa Bahi.

Sauti ya Mzee Ramadhani Issa mwenyeji na mkazi wa Bahi
Jengo l a ofisi ya Mkuu wa Wilaya Bahi