Dodoma FM

Urejeshaji taka fursa mpya kwa vijana

10 September 2024, 7:22 pm

Picha ikionesha taka zinazoweza kurejelezwa na kuzalisha bidhaa zingine

Na Mariam Kasawa.

Mahfoudh Haji ni makamu mwenyekiti wa taasisi ya Green Samia Foundation anasema taka ni fursa hasa kwa vijana lakini uelewa bado ni mdogo kwani wengi wanaamini waokota taka rejeshi ni watu duni hivyo kuidharau kazi hii. Kutokana na dhana hii, wamejipanga kutoa taaluma ya urejeshaji taka kwa vijana kama fursa mpya ya kiuchumi.

Sauti ya Bwn, Mahfoudh Haji

Makamu mwenyekiti wa taasisi ya Green Samia Foundation anasema taka zina faida kubwa kijamii na kiserikali.

Sauti ya Bwn, Mahfoudh Haji

Wadau wa mazingira wanaeleza kuwa licha ya kwamba taka hasa taka rejeshi zinaweza kuwa sehemu ya fursa na kumwingizia kipato mtu lakini jamii hasa vijana waliopo vyuoni bado hawatambui fursa hizi.

Sauti ya mdau wa mazingira
Picha kuonesha taka rejeshi