Dodoma FM

Nala kusahau adha ya maji

6 September 2024, 9:03 pm

Na Mindi Joseph . Wakazi wa Nala wataondokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa sasa kutokana na kukosekana kwa huduma thabiti ya maji safi. Wakieleza kwa nyakati tofauti, gharama zianazowakabili ni pamoja na gharama kubwa ya kupata huduma ya maji toka kwa watu binafsi.

Sauti za wananchi

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Balozi Job Masima amesema kwa muda mrefu Kata ya Nala imekuwa na changamoto ya maji.  

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Balozi Job
Sauti ya Balozi Job

Balaozi Job amesema kuwa kwa sasa  DUWASA inataekeleza mradi wa ujenzi wa tanki la maji unaotarajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwezi wa kwanza mwaka 2025. Tanki hili lenye uwezo wa ujazo wa lita 200,000 za ujazo unatarajiwa kumaliza adha ya maji Nala.

Sauti ya Balozi Job
DUWASA inataekeleza mradi wa ujenzi wa tanki la maji lenye uwezo wa ujazo wa lita 200,000