Taka ni fursa kwa uwekezaji na ajira
5 September 2024, 8:02 pm
Bidhaa zinazozalishwa kutokana na taka za mifuko chakavu na plastiki cha Future Corolful kilichopo Jijini Dodoma
Na Mariam Kasawa. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muunganona Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amefanya ziara ya kukagua uzingatiaji wa sheria ya mazingira katika kiwanda cha kurejeleza taka za mifuko chakavu na plastiki cha Future Corolful kilichopo Jijini Dodoma na kuona bidhaa zinazotokaana na taka hizo.
Mhandisi Cyprian Luhemeja katibu mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) pamoja na kuelezea kwa kina bidhaa zinazotokana na taka zinazokusanywa kiwandani hapo, anasema wananchi wanapaswa kutambua kuwa taka ni mali na kufahamu fursa zinazo patikana kutokana na taka ngumu kupitia viwanda hivi vya urejereshaji wa taka nchini.
Aidha wamiliki wa viwanda nchini wametakiwa kutambua umuhimu wa kuweka mifumo ya majitaka kuepusha maji hayo yasitiririke ovyo na kuchafua mazingira kwa kuafuta njia bora ya kurejeleza maji hayo ili yatumike katika shughuli za viwanda hatua itakayo wapunguzia gharama ya upatikanaji wa maji .
Aidha amewataka wamiliki kuhakikisha taka zote zinazo kusanywa na kurundikwa sehemu moja kwa ajili ya kurejelesha wahakikishe wanazifunika na kuhakikisha wafanyakazi wake wanakuwa na vifaa vya kujikinga kutokana na kugusa au kunusa taka zinazo kusanywa ili kulinda Afya zao.