Kampeni ya kutokomeza njaa, utapiamlo kuzinduliwa Septemba 6
3 September 2024, 4:53 pm
Hili ni Jukwaa la nne kuwakutanisha mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kila mwaka tangu kuanza kufanyika mwaka 2021 ambapo mwaka huu mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Doto Biteko .
Na Mariam Matundu.
Kampeni ya kutokomeza njaa na utapiamlo kwa watoto inatarajiwa kuzinduliwa Septemba sita mwaka huu ambapo wizara za kisekta zitatoa matamko mbalimbali yanayolenga kutekeleza kampeni hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea katika jukwaa la mwaka la mashirika yasiyokuwa ya kiserikali linalotarajia kuanza Septemba 04 hadi 06 mwaka huu hapa Dodoma, Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mwanaidi Ali Khamisi amesema jukwaa hilo ni muhimu kwa mustakabali wa maendeleo.
Kwa upande wake Meneja Kitengo cha Uchechemuzi na Jinsia kutoka World Vision Tanzania Esther Mongi amesema kampeni hiyo ya kutokomeza njaa na utapiamlo kwa watoto itaanza kutekelezwa katika mikoa 16 ya Tanzania.
Amesema kuwa kupitia jukwaa hilo la mashirika yasiyokuwa ya kiserikali wanaamini wataweza kupata ushirikiano wa kutoka kwa wadau mbalimbali ambao watasaidia kutekeleza kampeni hiyo yenye kaulimbiu ‘’INATOSHA WATOTO WOTE TANZANIA BILA UTAPIAMLO INAWEZEKANA CHUKUA HATUA’’