DUWASA yashauriwa kutatua kero za maji kwa wananchi
3 September 2024, 5:12 pm
Na Yusuph Hassan.
Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mkoani Dodoma DUWASA imeshauriwa kuanzisha dawati kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za maji kwa wananchi.
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Janet Mayanja akizungumza katika Kikao kazi kati ya duwasa na viongozi wa serikali za mitaa kujadili masuala ya huduma za maji kilichofanyika ndani ya wilaya ya chamwino.
Aidha ameshauri pia DUWASA kushirikiana na taasisi nyengine ikiwemo Tanesco, Tarura na Tanroad ili shughuli hizo katika utendaji wake zisiathiri mifumo yamaji.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa DUWASA Mhandisi Aaron Joseph amesema kikao hicho kitasaidia kupata Mawazo Chanya huku meneja wa DUWASA Kanda ya Chamwino George Mwakamele mambo yaliyofanyika katika sekta ya maji tangu wilaya ya chamwino kukubidhiwa kwa DUWASA.
Nao baadhi ya washiriki wa kikao hicho wametoa maoni yao juu huduma ya maji namna inavyopatikana katika wilaya hiyo.
Wilaya ya Chamwino ni miongoni mwa wilaya zinazohudumiwa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Duwasa katika Vijiji Vitano ikiwemo kata ya Chamwino, kata ya Buigiri, kata ya Msanga tangu mwaka 2020 mpaka 2024.