Lishe ni muhimu kwa ufaulu wa wanafunzi
2 September 2024, 5:32 pm
Licha ya kuimarisha kinga ya mwili lishe bora pia inaelezwa inatajwa kumsaidia mwanafunzi kuwa na uwezo wa kufikiri na kumbukumbu hivyo kumwezesha mwanafunzi kuelewa na kukumbuka masomo kwa wepesi.
Na Mindi Joseph.
Imeelezwa kuwa Mpango Mkakati wa Afya na lishe shuleni una mchango mkubwa katika kuimarisha Afya na ufaulu kwa wanafunzi.
Katika mahojiano na Mratibu wa Programu ya Elimu ya Afya na Ustawi kutoka UNESCO Mathias Faustine amesema katika kuhakikisha ubora wa elimu kwa watoto na vijana shuleni lazima pawe na lishe bora.
Kwa upande wake Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Afya Shuleni kutoka Wizara ya Afya Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma Beauty Mwambebule amesema mlo sahihi shuleni ni suala muhimu.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma kutoka Wizara ya Afya Dkt. Norman Jonas amesema miaka mitano ijayo kutakuwa na mabadiliko kupitia mpango wa kuboresha afya za wanafunzi kuanzia shuleni hadi vyuoni.