Dodoma FM

Wananchi watoa maoni mapendekezo bei mpya ya umeme

2 September 2024, 10:59 am

This image has an empty alt attribute; its file name is images-2022-01-05t135938519.jpg
Picha ni fundi umeme akifanya marekebisho ya nyaya katika nguzo ya umeme. Picha Swahili times,

Kwa sasa bei za Uniti za Umeme Nchini Tanzania zinatofautiana kulingana na matumizi na Ruzuku za Serikali.

Na Seleman Kodima.

Wakazi wa Jiji la Dodoma wamekuwa na maoni tofauti juu ya mapendekezo yaliyotolewa Bungeni Jijini Dodoma juu ya mapatio mapya ya bei ya Umeme kwa watumiaji kufuatia Mradi wa kufua Umeme wa Julius Nyerere kukamilika.

Wakizungumza na Dodoma FM Wananchi hao wamesema endapo Serikali itaangalia upya bei za uniti za Umeme itapunguza kero zitazotokana na gharama za Umeme.

Sauti za wananchi.

Kwa sasa bei za Uniti za Umeme Nchini Tanzania zinatofautiana kulingana na matumizi na Ruzuku za Serikali kwa wastani, bei ya Uniti moja ya Umeme yenye Ruzuku ni Sh100 kwa matumizi ya kawaida chini ya Uniti 75 kwa mwezi bila Ruzuku bei hiyo ni Shilingi 2921.