TANESCO Kufanya maboresho ya mfumo wa mita Kanda ya Kati na Kaskazini
20 August 2024, 4:55 pm
Zoezi la maboresho ya mfumo wa mita za LUKU limeshafanyika katika kanda tofauti hapa nchini ambapo ukomo wa zoezi hilo ni Novemba 24 mwaka huu.
Na Selemani Kodima.
Shirika la Umeme Tanzania TANESCO limesema linatarajia kufanya maboresho ya mfumo wa mita za luku kwa Kanda ya Kati na Kanda ya Kaskazini ikiwa lengo ni kuendana na viwango vya mfumo wa luku kimataifa.
Akitoa taarifa hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanesco mbele ya waandishi wa Habari Kaimu mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Irene Gowelle amesema lengo la maboresho hayo ni kuongeza ufanisi na usalama wa mita za luku nchini.
Aidha Gowelle amewatoa hofu wananchi na kuwataka wananchi kuendelea kununua umeme ili kuweza kufanya maboresho hayo .
Zoezi la maboresho ya Mfumo wa Mita za luku limeshafanyika katika kanda tofauti hapa nchini ambapo ukomo wa zoezi hilo ni november 24 mwaka huu.