Mchango wa wazazi ,walezi, jamii kuhakikisha uwepo wa mazingira rafiki ya kupata elimu
16 August 2024, 2:40 pm
Leo tunakupa Taarifa hiyo yenye kuonesha umuhimu wa kuchagia ujenzi wa Mabweni kwa ajili ya kupunguza changamoto hiyo ambayo inachangia kupoteza ndoto za mabinti wengi.
Na Seleman Kodima.
Ikumbukwe Mazingira rafiki kwa Mtoto wa kike kupata elimu yamezidi kuwa changamoto ya maendeleo kwake na taifa kwa Ujumla.
Umbali kutoka nyumbani hadi shuleni (shule hazina mabweni) wasichana wanatembea zaidi ya km10 kwa siku kuitafuta elimu.
vishawishi na misaada yenye nia ovu njiani; wanakutana na mazingira yasiyo rafiki ya kujifunzia shuleni toka kwa walimu, wanafunzi na jamii kwa ujumla.
kutokana na Mazingira hayo yanasababisha Binti huyu kupata mimba ,kubakwa, Ku kulaghaiwa, kushawishika kutokana na shida zinazomzunguka