Dodoma FM

Nini kifanyike TASAF iwafikie walengwa sahihi?

16 August 2024, 1:51 pm

Picha ni baadhi ya wakazi wa jiji la Dodoma wakiongea na Dodoma Tv kuhusu mfuko wa TASAF.Picha na Fred Cheti.

Dodoma TV Imepita Mtaani Kuzungumza na baadhi ya hapa Wananchi Jijini Dodoma kuhoji je nini kifanyike ili wanufaika wa Mfuko huo wawe ni walengwa sahihi.

Na Fred Cheti.
Kulingana na Takwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS asilimia nane ya Watanzania wadaiwa kuwa na umasikini uliokithiri jambo ambalo lilipelekea kuanzishwa kwa Mpango wa kunusuru kaya masikini kupitia (TASAF) Mnamo mwaka 2000.

Baada ya kuanzishwa kwa Mpango huo kumekua kukiibua madai mbalimbali kuwa baadhi ya wanufaika wa Mfuko sio walengwa sahihi kutokana na sababu mbalimbali jambo ambalo limekua likileta sintofahamu kwa Jamii.

Sauti za wananchi.
Picha ni Afisa mahusiano kutoka katika Mfuko huo.Picha na Fred Cheti.

Mpaka sasa Mfuko huo wa Maendeleo ya Jamii kupitia Mpango huo wa kusaidia Kaya Masikini unatajwa kuhudumia Kaya Milioni 1.3 kama ambavyo anabainisha Afisa mahusiano kutoka katika Mfuko huo.

Sauti ya Afisa mahusiano.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilianza kutekeleza Mradi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii – TASAF kuanzia mwaka 2000, ikiwa ni moja ya mbinu za kutokomeza umasikini ambazo zilisaidia Ajenda ya ugatuaji wa Madaraka kwenye kipindi cha 2009 – 2012, TASAF ilifanya majaribio ya uhawilishaji fedha taslimu kwa masharti nafuu.