Tumieni sherehe za jando kufundisha maadili na tamaduni za kitanzania
16 August 2024, 1:26 pm
Sherehe hizo ni sehemu pekee ya kuwamsaidia Kijana kupata ufahamu wa namna ya kukabiliana na changamoto za Maisha katika siku za usoni.
Na Kadala Komba.
Wakazi wa Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma wametakiwa kuzitumia Sherehe za Jando kwa Watoto wa kiume kwa ajili ya kutoa Elimu juu ya maadili na Tamaduni za Kitanzania.
Afisa utamaduni sanaa na Michezo wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Recho Mwitula ametoa wito huo wakati akizungumza na taswira ya Habari Ofisini kwake juu ya uwepo wa Sherehe ya Jando kwa Watoto wa kiume.
Kwa upande wake Andrea Shamba ambaye ni Mzazi wa Watoto waliofanyiwa Jando uendelezaji wa Utamaduni huo unasaidia kuwaepusha Watoto na Tamaduni za ambazo hazina maadili katika Jamii.
Ndugu wa karibu wa Familia ya Watoto waliofanyiwa Tohara akiwemo Happiness Mpangwa na Elias Tomas wameeleza namna utaratibu wa kushiriki sherehe hiyo unavyofanyika.