Wakazi Mchito watatuliwa kero ya maji
15 August 2024, 5:44 pm
Baadhi ya wananchi hao wametoa shukrani zao za dhati kwa shirika hilo kwani kupitia msaada wa kisima kirefu cha maji kimepelekea wananchi kujikita na kilimo cha umwagiliaji.
Na Victor Chigwada.
Wananchi wa kijiji cha Mchito wametoa shukrani kwa wadau na wahisani ambao wameweza kuwa mstari mbele kuwatatulia changamoto ya maji kwa kuwajengea kisima.
Pongezi hizo zimetolewa na baadhi ya wakazi wa Mchito ambapo wamesema shirika la Innovation of Africa limeendelea kuwa nuru kwa jamii ya watu waishio vijijini na hata mijini kutokana na jitahada kubwa wanazozifanya katika kuwasaidia wananchi.
Aidha wamesema shughuli hizo zimekuwa na tija kwao kwani zinawasaidia kuongeza kipato na kuendesha maisha yao ya kila siku.
Abduli Mateke ni Mwenyekiti wa eneo hilo amesema kuwa kisima hicho kimekuwa ni fursa kwao hasa kwenye shughuli za kila siku za wananchi.
Hata hivyo ameendelea kuwaomba wadau wa kilimo kufika Msisi na kutoa elimu zaidi juu ya kilimo bora na chenye tija zaidi.