Vijana watakiwa kuhakikisha wanapata elimu ya afya ya uzazi
14 August 2024, 6:42 pm
Elimu ya afya ya uzazi kwa vijana ina umuhimu mkubwa kwa jamii katika kujiletea ustawi wake.
Na Witness Obeid.
Vijana waliopo masomoni wametakiwa kuhakikisha wanapata elimu ya afya ya uzazi kutokana na wengi wao kupata mabadiliko wakiwa bado masomoni.
Akizungumza na Dodoma TV mapema leo Afisa Elimu Kata ya Mbabala Jijini Dodoma, Mwalim Shaban Kijoji amasema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kutoa Elimu hiyo kwani inawasaidia kupunguza Mimba za Utotoni.
Francis Andrew Daktari kutoka Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (UMATI) amesema kuwa mwitikio wa Vijana katika Jamii ni mdogo ingawa Serikali inajitahidi kuhakikisha inafikisha Elimu hiyo kwa Vijana wa rika zoe.
Kwa upande wao baadhi ya Vijana waliopata Elimu ya Afya ya uzazi wamesema Elimu hiyo inawasaidia kutimiza malengo yao hasa katika Elimu na husidia kujikinga na Mimba za Utotoni.
Hivi karibuni Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma wa Wizara ya Afya Dkt. Tumaini Haonga amesema Elimu ya Afya ya Uzazi kwa Vijana ina umuhimu mkubwa kwa Jamii katika kujiletea ustawi wake na kwa kutambua hilo Wizara ilianzisha Kituo cha Simu cha Wizara ya Afya( Afya Call Centre 199 ) pamoja na mambo mengine ili pia kuwasadia Vijana kupata Elimu juu ya masuala ya Afya.