Dodoma FM

Wawekezaji watakiwa kufanya tathmini ya athari kwa mazingira

13 August 2024, 4:36 pm

Picha ni moja miradi ya wawekezaji inayo endelea .Picha ni NEMC.

Tathmini ya athari kwa mazinngira na jamii inajumuisha tathmini mbalimbali, kuanzia uchanganuzi wa bioanuwai na ubora wa maji hadi athari za matumizi ya ardhi na jamii ya wenyeji wa eneo husika.

Na Mariam Kasawa.
Wawekezaji wametakiwa kufanya tathmini ya athari kwa mazingira na jamii kabla ya kuwekeza mradi wowote ili kuepuka hasara na migogoro.

Tathmini ya athari kwa mazingira ni michakato ya kimfumo iliyoundwa kutambua na kutabiri matokeo ya kimazingira ya miradi na hatua zinazopendekezwa.

Lengo ni kutathmini athari zinazoweza kutokea kwa mazingira kabla ya kufanya uamuzi wowote na kutafuta njia za kupunguza, kupunguza au kuepuka athari mbaya zinazoweza kujitokeza.

Bi. Lilian Lukambuzi mkurugenzi wa tathmini ya athari kwa mazingira na Jamii anasema miradi mingi inayo wekezwa bila kufanya tathmini hupata atari mbalimbali ikiwemo kuvamiwa na wananchi kutoka na kukosa taarifa kuhusu mradi husika.

Sauti ya Bi Lilian Lukambuzi.
Picha ni moja miradi ya wawekezaji inayo endelea .Picha ni NEMC.

Tathmini ya Athari kwa Mazingira ni muhimu sana kwa kusawazisha maendeleo ya kiuchumi na utunzaji wa mazingira ya eneo husika.

Licha ya kwamba tathmini zinasaidia mazingira ya karibu na mradi kuwa salama je ni zipi faida zake nyingine huyu hapa Bw.Abel Sembeka meneja wa Nemc kanda ya Morogoro.

Sauti ya Bw.Abel Sembeka.