Dodoma FM

Wanufaika mradi wa BBT waishukuru serikali

13 August 2024, 3:47 pm

Picha ni Naibu waziri wa Kilimo Mh. Anthony Mavunde katika picha ya pamoja na vijana waliopo katika mafunzo ya Kilimo chini ya Programu ya Building A Better Tomorrow (BBT) katika kituo cha Mafunzo cha Bihawana-Dodoma.Picha na Halmashauri ya jiji la Dodoma.

Zaidi ya vijana 110 kutoka mradi wa BBT chinangali wamenufaika na mikopo ya uendeshaji wa shughuli hiyo ya kilimo wenye thamani zaidi ya milioni 900 huku zaidi ya hekari 600 zikiwa tayari zimeshalimwa zao la alizeti.

Na Victor Chigwada.
Vijana wanufaikaji wa mafunzo ya mradi wa BBT kutoka Chinangali Kata ya Majeleko wameishukuru Serikali kwa fursa hiyo ambayo wanaamini itabadilisha maisha yao.

Hayo wameyaeleza wakati wakizungumza na Taswira ya Habari kuhusu namna walivyojikita na kilimo baada ya kupata mafunzo ambayo yanalenga kilimo che Tija.

Baadhi yao wamesema kuwa fursa hiyo ni muhimu kuitumia kwani tayari imekuwa ni silaha kwa vijana wasio na ajira nchini.

Sauti za wananchi.
Picha ni Naibu waziri wa Kilimo Mh. Anthony Mavunde katika picha ya pamoja na vijana waliopo katika mafunzo ya Kilimo chini ya Programu ya Building A Better Tomorrow (BBT) katika kituo cha Mafunzo cha Bihawana-Dodoma.Picha na Halmashauri ya jiji la Dodoma.

Aidha kupitia maadhimisho ya vijana yaliyo fanyika Dodoma kitaifa na kuhudhuriwa na Waziri wa Nchi ,ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Vijana,ajira Wenye Ulemavu)Mh.Ridhiwani Kikwete hapo jana ameewaahidi vijana kuwa Serikali itaendelea kuwa nao bega kwa bega ili kuhakikisha wanakuwa na tija ya kuchangia maendeleo ya nchi yao.

Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuhakikisha inaboresha na kutoa mafunzo ambayo yataendana na teknolojia ya kidijitali nchini.

Sauti ya Mh.Ridhiwani Kikwete.