Dodoma FM

Sumu kuvu hatari kwa afya, uchumi

12 August 2024, 4:57 pm

Picha ni Bi. Ester Masao Afisa Mdhibiti Ubora katika mradi wa kudhibiti sumu kuvu nchini TANPAC. Picha na Mariam Kasawa.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), sumu kuvu huharibu karibu asilimia 25 au zaidi ya chakula kinachozalishwa duniani kila mwaka.

Na Mariam Kasawa.
Imeelezwa kuwa sumu kuvu ina athari kwa afya za wananchi na uchumi kwa ujumla kama wakulima watashindwa kuzingatia kanuni bora za kilimo.

Bi. Ester Masao Afisa Mdhibiti Ubora katika mradi wa kudhibiti sumu kuvu nchini TANPAC anasema sumu kuvu ina madhara makubwa kwa afya na uchumi wa taifa endapo mkulima hatazingatia mbinu bora za kilimo na uhifadhi bora wa mazao baada ya kuvuna.

Sauti ya Bi Ester Masao.

Aidha Bi Ester anasema endapo mkulima ataona dalili mazao yana viashiria vya sumu kuvu asimpatie mnyama na aepuke kutupa katika mazingira badala yake ayateketeze kwa moto au kuyafukia katika shimo.

Sauti ya Bi Ester Masao.