Dodoma FM

Dawati la sekta binafsi la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwainua vijana

12 August 2024, 4:42 pm

Picha ni Deogratis Gambango Mratibu mkuu wa dawati hilo kutoka wizara ya mifugo na uvuvi.Picha na Fred Cheti.

Ni changamoto ipi inapelekea jamii hasa vijana kutojiingiza katika sekta ya mifugo na uvuvi.

Na Fred Cheti.
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeanzisha dawati la sekta binafsi kwa lengo kuangalia changamoto inayokwamisha jamii wakiwemo vijana kujihusisha na shughuli ya ufugaji inayotajwa kuwa na manufaa makubwa.

Hayo yameelezwa na Deogratis Gambango Mratibu Mkuu wa dawati hilo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati akifanya mahojiano na Dodoma TV kuhusu fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya mifugo na uvuvi ambayo inatajwa kuchangia uchumi wa taifa kwa asilimia 7.

Sauti ya Bw.Deogratis Gambango.
Picha ni Dkt. Pius Mwambege mtendaji mkuu wa wakala wa mafunzo ya mifugo na vuvi feta.Picha na Fred Cheti.

Miongoni mwa changamoto inayosababisha jamii hasa vijana kutokuingia katika sekta ya mifugo na uvuvi ni ujuzi lakini zipo taasisi zinazotoa mafunzo katika sekta hiyo na hapa Dkt. Pius Mwambege mtendaji mkuu wa wakala wa mafunzo ya mifugo na vuvi Feta anatolea ufafanuzi.

Sauti ya Dkt. PiusMwambege .

Dodoma Tv imezungumza na baadhi ya wananchu jijini dodoma akiwemo Aman John pamoja na Issa Rashid ambapo wameeleza ili kuwavutia vijana katika sekta hiyo elimu inatakiwa kuendelea kutolewa kwao.

Sauti za vijana.