Dodoma FM

Toam yaanzisha mkakati wa kilimo ikolojia hai

7 August 2024, 6:00 pm

Picha ni Msimamizi wa miradi kutoka Shirika la Kilimo hai Tanzania Brigita Didas Masawe.Picha na Shangwe.

Shirika la Kilimo Hai Tanzania Toam lenye makao yake makuu Jijini Dare s salaam limefanikiwa kufungua matawi yake katika maeneo mbalimbali Nchini ikiwemo Mkoa wa Dodoma.

Na Shangwe.
Shirika la Kilimo Hai Tanzania Toam limeanzisha mkakati wa Kilimo ikolojia Hai Tanzania ambao unalenga kukuza na kusimamia Kilimo hai Tanzania ukiwa na malengo 12.

Msimamizi wa miradi kutoka Shirika la Kilimo hai Tanzania Brigita Didas Masawe amebainisha hayo wakati akizungumza na Dodoma TV katika maonesho ya Kimataifa ya Nanenane yanayoendelea katika VViwanja vya Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma.

Hata hivyo Brigita amesema mkakati huo unahusisha Wananchi wote wenye mawazo ya kuboresha Sekta ya Kilimo hivyo ni fursa kwa kila mmoja kujitokeza kutoa maoni yake kwa ajili ya kutekeleza mkakati huo.

Sauti ya Brigita Didas Masawe.
Wananchi wote wenye mawazo ya kuboresha Sekta ya Kilimo hivyo ni fursa kwa kila mmoja.Picha na Shangwe.

Brigita amewakaribisha Watanzania wakiwemo Wakazi wa Dodoma kufika katika Banda la Toam lililopo katika maonesho ya Nanenane Jijini Dodoma kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo usalama wa Chakula Tanzania.

Sauti ya Brigita Didas Masawe.